NA DIRAMAKINI
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imetangaza kwa masikitiko makubwa kifo cha Mtumishi wake, Bw. Julius Hans Ntullo, aliyekuwa akihudumu katika Idara ya Utawala na Utumishi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Jiji hilo, marehemu alifariki dunia tarehe 20 Machi 2026 katika Hospitali ya Kisarawe baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa,taratibu za mazishi zinaendelea kufanyika nyumbani kwa marehemu, kilichopo Chanika-Buyuni, jijini Dar es Salaam.
Aidha, mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika tarehe 23 Machi 2026 katika eneo hilo la Chanika.
Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imetoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa na wafanyakazi wote walioguswa na msiba huo, huku ikiwataka kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu.
“Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe,” imehitimisha taarifa hiyo.
