Viongozi wa Mawasiliano Serikalini wakutana kujadili utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050

DODOMA-Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Fedha, Bw. Benny Mwaipaja amekutana na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka Ofisi ya Rais-Mipango na Uwekezaji, Bw.Titus Kaguo, baada ya kumtembelea katika ofisi zake zilizopo Wizara ya Fedha (Treasury Square) jijini Dodoma.
Katika kikao hicho, viongozi hao walijadili masuala mbalimbali yanayohusu uratibu na uimarishaji wa mawasiliano ya Serikali kwa lengo la kuhakikisha taarifa muhimu za maendeleo ya taifa zinawafikia wananchi na wadau kwa ufanisi.

Aidha, mazungumzo yao yalijikita katika kupanga mikakati ya ushirikiano kati ya taasisi hizo mbili ili kuimarisha utoaji wa taarifa sahihi kuhusu utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.
Pia,viongozi hao walikubaliana kuendeleza ushirikiano wa karibu katika kubuni na kutekeleza mikakati ya mawasiliano itakayosaidia kuongeza uelewa wa wadau kuhusu Dira hiyo pamoja na kuhamasisha ushiriki wao katika kuifanikisha kwa manufaa ya maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here