MANYARA-Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba amepokea kero na hoja mbalimbali 305 kutoka kwa wananchi wa Wilaya ya Mbulu akiwa kwenye mkutano wa hadhara ambao ni wa mwisho katika ziara ya kikazi ya siku tatu ya Mkoa wa Manyara.
Akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali leo jioni Machi 2, 2026 katika uwanja wa mpira wa Mbulu Mjini, Waziri Mkuu amesema anataka kuona utaratibu wa kulundika kero za wananchi unaisha mara moja.
“Kila mtu aliyeko ofisini anapaswa ajishughulishe na mambo yanayowahusu wananchi. Ninaandaa utaratibu, kila mwisho wa mwezi kila mtu atapaswa kutoa taarifa ametatua kero ipi na ipi imeshindikana kuanzia kijiji na mtaa, kata, tarafa, wilaya hadi mkoa. Tutafuatilia utekelezaji wake,” amesema.
Dkt. Mwigulu amesisitiza kuwa hilo siyo la suala la ziara tu bali anataka wananchi wakifika kwenye ofisi za viongozi wapewe vitabu vya wageni na waandike hoja zao ili iwe rahisi kufuatilia utekelezaji wake.
Amesema kuwa mambo ya kupuuza na kuzoea shida za wananchi siyo makusudi ya kuanzishwa kwa ofisi za umma. “Tunataka watumishi wajihusishe na matatizo ya wananchi. Tulianzisha ofisi siyo kwa ajili ya kugawana madaraka, bali watafute ufumbuzi wa matatizo ya wananchi. Tunataka mambo ambayo yanaweza kufika ukomo yaishe,” amesisitiza.

Akiwa njiani kuelekea Mbulu mjini, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alikagua ujenzi wa barabara ya km 25 kutoka Mbulu hadi Garbabi ambayo ni sehemu ya barabara kuu inayojengwa kwa kiwango cha lami kutoka Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa yenye urefu wa km 389.
Utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 41.7 ambapo sh. bilioni 36.3 zitatumika kukamilisha ujenzi. Hadi sasa, sh. bilioni 12.5 tayari zimeshalipwa.
Mradi huo unaotekelezwa na Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) unalenga kuboresha mawasiliano ya barabara, kuimarisha usafirishaji wa watu na bidhaa, na kuchochea ukuaji wa uchumi katika maeneo husika.
Mapema, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga alisema kwa mara ya kwanza wameandika historia ya kushika namba mbili kitaifa kwenye matokeo ya kidato cha nne ya mwaka jana. “Hii ni historia, haijapata kutokea,” alisema.
“Huu si muujiza bali ni majibu ya jitihada za Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika elimu kwa kujenga shule za msingi na sekondari, madarasa mapya na mabweni ili kupunguza umbali kwa watoto hasa wanaotoka kwenye jamii za wafugaji,” alisema.