Wizara ya Fedha yawakutanisha wataalam kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti ya Sekta ya Elimu

DODOMA-Wizara ya Fedha kupitia Idara ya Usimamizi wa Bajeti ya Serikali, imefanya kikao kazi cha wataalam wa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kwa ajili ya kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti ya Sekta ya Elimu (inayosimamiwa na Wizara ya Elimu pamoja na Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI)) ili kuhakikisha kuwa yanazingatia vipaumbele na Mipango ya Taifa, sera na mikakati ya maendeleo, pamoja na miongozo ya upangaji na uandaaji wa bajeti.
Kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma na kufunguliwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara hiyo, Lusius Mwenda kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ni sehemu muhimu ya mchakato wa maandalizi ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027, kinalenga kupitia, kuchambua na kujadili mipango na mapendekezo ya bajeti yaliyowasilishwa na sekta mbalimbali ili kufanya tathmini ya kina ya maeneo muhimu ya vipaumbele katika Bajeti ya Mwaka 2026/2027, uhusiano wa Sera na namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya sekta, mikakati mipya ya kisera, ulinganifu wa Mpango Mkakati (SP) na Dira ya Taifa 20250, Mpango wa Nne wa Maendeleo wa Taifa (FYDP IV) pamoja na Mpango wa Maendeleo wa Mwaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here