Wizara ya Habari yapatiwa shilingi bilioni 50 kuwawezesha vijana nchini

ARUSHA-Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imetangaza uwepo wa mfuko wa jumla ya Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wanaojihusisha na sekta ya ubunifu nchini ikiwemo watengeneza maudhui mtandaoni (content creators), wasanii, wanamuziki, waigizaji, waandishi wa habari, influencers pamoja na wabunifu wa kazi mbalimbali za sanaa.
Akizungumza jijini Arusha Machi 11, 2026, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda amesema mfuko huo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, yenye lengo la kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sekta ya habari, sanaa na ubunifu.
Waziri Makonda amesema awali Wizara ilikuwa imepangiwa Shilingi Bilioni 20, lakini baada ya mazungumzo na Benki ya CRDB, kiwango hicho kimeongezwa na kufikia jumla ya Bilioni 50 ili kupanua wigo wa vijana watakaonufaika na mfuko huo.

Ameeleza kuwa kwa sasa kinachosubiriwa ni tarehe rasmi ya uzinduzi wa mfuko huo, ambapo baada ya uzinduzi fedha hizo zitaanza kutolewa kwa vijana waliopo katika sekta ya habari, sanaa na ubunifu ili kuwawezesha kukuza kazi zao na kuchochea maendeleo ya uchumi wa taifa.

Wizara inapanga kuzindua rasmi mfuko huo katika hafla maalum inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi wa uzinduzi huo.
Hatua hiyo inaelezwa kuwa sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha vijana wanapata fursa za kiuchumi na kutumia vipaji vyao kama chachu ya maendeleo ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here