Chakwera akutana na Tume ya Uchunguzi

DAR-Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola, na Rais mstaafu wa Malawi,Dkt. Lazarus Chakwera, amekutana na kufanya Mazungumzo na Tume ya uchunguzi wa Matukio ya vurugu za Uchaguzi na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29,2025.
Ujumbe huo wa Jumuiya ya Madola umekutana na Tume hiyo katika ofisi zao zilizopo jijini Dar es Salaam mapema hii leo.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Othuman Chande amesema, mazungumzo yao yalijikita zaidi kueleza shughuli za tume hiyo na Hadidu za rejea za tume.

Chakwera anaendelea na ziara yake ya kikazi ambayo anatarajia kuhitimisha Aprili 16,mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here