Hakuna jambo la ajabu kuwa Mbunge, Watanzania wamekupa imani tu-Dkt.Biteko

GEITA-Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt.Doto Biteko amewaomba wanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Geita, kuwafundisha wabunge wao kuwa bora.
Dkt.Biteko ameyasema hayo Aprili 19, 2026 katika Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Chama hicho Mkoa wa Geita, uliofanyika katika viwanja vya ofisi mpya za CCM Mkoa.

"Hakuna jambo la ajabu kuwa Mbunge bali Watanzania wamekupa imani tu,”amesema.

Dkt.Biteko ameongeza kuwa Mbunge bora na mbaya anatengezwa na wapiga kura wake, hivyo wasiache kuwakosoa pale wanapofanya vibaya ili wawe Bora zaidi.

Aidha, Dkt. Biteko amewaomba wabunge wa majimbo mengine ya Mkoa wa Geita, kuwaunganisha wananchi kwa kuwaweka katika uelekeo mmoja wa maendeleo na sio kuwagawa makundi makundi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here