Tanzania kuongeza ufanisi wa Bunge kupitia mafunzo ya IPU

ISTANBUL-Tanzania imesema ushiriki wake katika Mkutano Mkuu wa 152 wa Muungano wa Mabunge Duniani (IPU) unaoendelea Istanbul, Uturuki unalenga kujifunza mbinu bora zitakazosaidia kuboresha maisha ya wananchi.
Akizungumza akiwa nchini Uturuki leo, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo amesema,uzoefu unaopatikana katika mkutano huo ni muhimu kwa maendeleo ya wananchi.
"Ushiriki wetu katika IPU unatusaidia kujifunza mifano bora ya kimataifa ambayo tutaitumia kuboresha utungaji wa sheria na huduma kwa wananchi ili kuleta maendeleo ya moja kwa moja,”amesema Sillo.

Amesema,mijadala ya kimataifa inasaidia Bunge kuimarisha utendaji wake na kuongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.

Tanzania pia inajiandaa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa 153 wa IPU utakaofanyika Arusha 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here