JWTZ latangaza nafasi za vijana kujiandikisha jeshini

NA DIRAMAKINI

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limetangaza nafasi za kuandikishwa jeshini kwa vijana wa Kitanzania wenye elimu kuanzia Sekondari hadi Elimu ya Juu.
Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa Aprili 14, 2026, waombaji wanatakiwa kuwa raia wa Tanzania, wenye afya njema, nidhamu nzuri na wasio na rekodi ya makosa ya jinai. 

Aidha, waombaji wanapaswa kuwa hawajawahi kutumikia vyombo vya ulinzi na usalama na wawe wamehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT).

JWTZ imesema vijana watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo ya kijeshi pamoja na fursa ya kuendeleza taaluma zao.

Kwa upande wa umri, waombaji wenye elimu ya Kidato cha IV na VI hawapaswi kuzidi miaka 25, huku wale wenye elimu ya juu wakitakiwa kutokuwa zaidi ya miaka 28.

Maombi yanapaswa kuandikwa kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi, Msalato jijini Dodoma kuanzia Aprili 15 hadi Aprili 28, 2026, yakifuatana na nyaraka muhimu ikiwemo kitambulisho cha taifa, vyeti vya elimu na cheti cha kuzaliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

1 Comments

  1. KWA WAITIMU WA KIDATO CHA NNE TU,
    ANARUHUSIWA KUJIUNGA{KUTUMA MAOMBI}
    IKIWA ANA VIGEZO VYOTE VILIVYO TAJWA ISIPO KUWA 👉AJAPITIA JKT
    👇
    Yani ana uraia wakuzaliwa na {vitambulisho vote NIDA,KURA n.k.}
    Afya nzuri {fitness}
    Nidhamu ya juu

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here