Magazeti leo Aprili 11,2026

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewapatanisha waimbaji wa muziki wa Injili Upendo Nkone na Martha Mwaipaja kufuatia mvutano wao uliokuwa ukiendelea na kujitokeza zaidi katika mitandao ya kijamii.
Mkutano huo ulifanyika Aprili 10, 2026 katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ambapo Chalamila alisema aliamua kuingilia kati baada ya kuona mgogoro huo ukichochea mgawanyiko miongoni mwa mashabiki na jamii kwa ujumla.

Alisisitiza kuwa wasanii hao wana ushawishi mkubwa katika jamii, hivyo wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa kudumisha amani, umoja na mshikamano.

Chalamila alisema aliwachukulia wasanii hao kama watumishi wenye vipawa vya kipekee, na akaona ni muhimu kuwakutanisha ili kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo ya moja kwa moja.

Hatua hiyo imekuja wakati mjadala wao ukiendelea mitandaoni, huku wadau wakihimiza maridhiano ili kulinda taswira ya muziki wa Injili nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here