Tanzania na Kenya zaimarisha ushirikiano wa kimkakati kukuza biashara na ujumuishaji wa kikanda

TANZANIA na Kenya zimethibitisha upya dhamira yao ya kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, huku viongozi wa nchi hizo mbili wakisisitiza kuongeza ushirikiano katika sekta za biashara, diplomasia na maendeleo ya kikanda.
Akizungumza katika mashauriano ya ngazi ya juu kati ya Wizara za Mambo ya Nje za nchi hizo mbili, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo, amesisitiza uimara wa ushirikiano huo unaotegemea maslahi ya pamoja na mifumo rasmi kama Tume ya Pamoja ya Ushirikiano (JCC) na Kamati za Pamoja za Biashara (JTC).

Amebainisha kuwa majadiliano yanayoendelea kati ya wizara mbalimbali na wataalamu yameweka msingi imara wa kuleta matokeo yenye tija, hasa katika sekta za nishati, usalama, viwanda na uwekezaji.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Masuala ya Diaspora wa Kenya, Dkt. Abraham Sing’Oei, ameeleza umuhimu wa kuendeleza zaidi ushirikiano wa kiuchumi, akibainisha kuwa biashara kati ya nchi hizo imevuka dola za Marekani bilioni moja, sambamba na kuongezeka kwa uwekezaji wa pande zote mbili.

Mkutano huo pia umejadili uondoaji wa vikwazo visivyo vya kikodi, huku pande zote zikiahidi kutatua changamoto zilizobaki ifikapo katikati ya mwaka 2026.

Aidha, mipango inaendelea ya kuitisha kikao cha Kamati ya Pamoja ya Biashara pamoja na jukwaa kubwa la wafanyabiashara litakalowakutanisha zaidi ya kampuni 200.
Majadiliano yamegusia pia ziara ijayo ya Kiserikali ya Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt. William Ruto, nchini Tanzania, ambapo atakutana na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa Tanzania, Bw. Ally Gugu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Aristides Mbwasi pia wameshiruki katika mkutano huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here