Magazeti leo Aprili 15,2026

Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI kwa kushirikiana na Shirika la Kuhudumia Watoto Ulimwenguni (UNICEF) inatoa mafunzo maalum kwa Maafisa Ustawi na Maafisa Lishe wa ngazi ya mkoa na halmashauri kutoka mikoa ya Dodoma na Dar es salam, ili kuwajengea uwezo wa kuandaa vifaa vya kujifunzia na kuchezea watoto kwenye vituo vya kulelea watoto wadogo mchana vilivyopo masokoni.
Mafunzo hayo kwa maafisa hao yameanza kutolewa Aprili 13, 2026 mkoani Morogoro, kwa lengo la kuwajengea uwezo utakaoimarisha ubora wa malezi na ujifunzaji kwa watoto wadogo katika ngazi za mikoa na halmashauri.

Akizungumzia mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo hayo kutoka OWM – TAMISEMI Bi Amina Mfaki amesema kuwa washiriki watapatiwa ujuzi wa kuandaa vifaa vya kujifunzia na kuchezea kwa kutumia rasilimali zinazopatikana katika mazingira yao, hatua inayotarajiwa kuongeza ubunifu, kupunguza gharama na kuhakikisha upatikanaji wa vifaa rafiki kwa watoto katika vituo hivyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here