Magazeti leo Julai 18,2026

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limeendelea kudhibiti vitendo vya uhalifu, baada ya kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa 200 katika operesheni maalumu zilizofanyika kuanzia Juni 1 hadi Julai 16, 2026.











Akizungumza Julai 17, 2026 Tanga, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, amesema kuwa Katika kipindi hicho cha wiki sita, jeshi hilo limebainisha kuwa hali ya ulinzi na usalama mkoani hapa ni shwari, huku likisisitiza kuwa mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano kati ya polisi na wananchi kupitia falsafa ya polisi jamii.

Katika hatua inayoashiria mwendelezo wa mapambano dhidi ya ukatili na uhalifu uliokithiri Kamanda huyo alisema kuwa jumla ya watuhumiwa 51 walitiwa hatiani na kuhukumiwa vifungo mbalimbali jela baada ya upelelezi wa kesi zao kukamilika.

Aliwajaka waliopewa adhabu kali ni Sadiki Waziri, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kusafirisha dawa za kulevya huku adhabu kama hiyo ya miaka 30 pia imewakuta Julius Mustafa (kwa kosa la kulawiti) na Kilimo Issaya (kwa kosa la kuzini na maharimu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here