Naibu Waziri Dkt.Ngwaru Maghembe awasili nchini Brazil kwa ziara ya kikazi

BRAZIL-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Dkt.Ngwaru Maghembe (Mb.) amewasili nchini Brazil kwa ziara ya kikazi.
Mhe.Naibu Waziri Dkt.Maghembe amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Dr. John Stephen simbachawene katika Ofisi ya Ubalozi. Mhe Naibu waziri alipata nafasi ya kukutana na kujadiliana masuala mbalimbali na Watumishi wa Ubalozi na kusisitiza umuhimu wa utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi kwa kuvutia uwekezaji kutoka Brazil.
Katika ziara hiyo Mhe.Dkt Ngwaru Maghembe (Mb.) ataongoza ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Mashauriano ya kisiasa kati ya Tanzania na Brazil. Mkutano huo unalenga kukuza uhusiano wa Kidiplomasia na Ushirikiano baina ya Tanzania na Brazili katika sekta mbalimbali ikiwemo biashara, Uwekezaji, Kilimo, Mifugo na Utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here