Naibu Waziri Millya awasilisha Salamu za Rais Samia kwa Mfalme Mswati III

MBABANE-Pembezoni mwa Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 40 ya Utawala wa Mfalme Mswati III, mjini Ezulwini, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, anayeshughulikia masuala ya Afrika Madhariki, Mhe. James Millya, amewasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Mfalme Mswati III wa Ufalme wa Eswatini.
Akipokea salamu hizo, Mfalme Mswati III amemshukuru Mhe. Dkt. Samia kwa salamu za pongezi na kueleza kuwa kitendo cha kutuma mwakilishi wake kwenye maadhimisho hayo ni ishara thabiti ya uhusiano mzuri na udugu uliopo kati nchi zote mbili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here