Profesa Luoga aipongeza Makumbusho ya BoT kwa utajiri wa maudhui Sekta ya Fedha na Uchumi nchini

DAR-Gavana Mstaafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Prof. Florens Luoga, ameimwagia sifa makumbusho ya Benki Kuu kwa kuwa na utajiri wa maudhui mbalimbali yanayoelezea historia ya fedha, historia ya Benki Kuu pamoja na mageuzi mbalimbali yaliyofanyika kwenye sekta ya fedha na uchumi wa nchi kwa ujumla.
Prof. Luoga alitoa sifa hizo alipotembelea Makumbusho ya Benki Kuu ambapo alipokelewa na Naibu Gavana wa BoT, Dkt. Yamungu Kayandabila, katika ofisi za Makao Makuu ndogo ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam Aprili 10 2026.

“Hongereni sana kwa kuanzisha makumbusho hii kwa kuwa ni kitu chenye upekee. Upekee wake ni kwamba Benki Kuu hapa nchini ipo moja tu,kwa hiyo maudhui yake lazima yawe na upekee na yenye maana kubwa kwenye historia ya nchi."
Alieleza kuwa makumbusho hayo yatanufaisha makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo watafiti, wanafunzi wa ngazi tofauti za elimu pamoja na wananchi kwa ujumla kwa kuwapatia fursa ya kujifunza historia ya fedha nchini na kuelewa mchango wa Benki Kuu katika kusimamia na kustawisha uchumi wa taifa katika vipindi mbalimbali vya mabadiliko ya kiuchumi tangu kuanzishwa kwake Juni 14 1966 hadi hivi sasa.

Pia, Gavana huyo mstaafu aliipongeza Benki Kuu kwa kutengeza makumbusho hayo kwa kutumia wataalamu wa ndani ya taasisi akitaja kitendo hicho kuwa ni cha kizalendo na kitapunguza utegemezi wa watoa huduma wa kigeni.

Katika hatua nyingine, Prof. Luoga alikutana na kufanya Mazungumzo na Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba.
Makumbusho ya Benki Kuu yalizinduliwa rasmi tarehe 30 Julai 2025 na Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Philip Mpango.

Makumbusho haya hufunguliwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa kuanzia 3:00 Asubuhi hadi saa 9:00 Alasiri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here