NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, jana Machi 31,2026 Ikulu jijini Dar es Salaam amekutana na wagombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, akiitikia wito wao wa kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu hali ya kisiasa na masuala ya maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Wagombea wa Nafasi ya Urais na Wagombea Wenza kutoka vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.
Viongozi hao kutoka vyama 16 vya siasa nchini walimtembelea Rais Dkt.Samia na kuwasilisha maoni yao kuhusu namna ya kuimarisha maridhiano ya kisiasa, demokrasia ya vyama, amani na mshikamano wa kitaifa baada ya Uchaguzi Mkuu, pamoja na namna ya kuimarisha ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo na kudumisha tunu za umoja wa kitaifa.
Majadiliano hayo pia yaligusia umuhimu wa kuendeleza maadili ya uongozi, uwajibikaji na siasa zenye staha, kama msingi wa kujenga Taifa lenye utulivu wa kisiasa na maendeleo endelevu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Wagombea wa Nafasi ya Urais na Wagombea Wenza kutoka vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025. Mazungumzo hayo yalifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais wa Vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais pamoja na Wagombea Wenza wa Vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya Mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.Katika kukuza demokrasia jumuishi, viongozi hao walisisitiza ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika masuala ya kitaifa na mchakato wa maendeleo, sambamba na kulinda utulivu wa kisiasa wakati wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kwa kutambua kuwa mazingira ya amani na umoja ni msingi wa ukuaji wa uchumi na ustawi wa wananchi.
Sambamba na hilo, walielezea umuhimu wa kuimarisha utamaduni wa uvumilivu wa kisiasa, kuheshimiana na kujenga uaminifu miongoni mwa wadau wa kisiasa, kama njia ya kuendelea kudumisha utulivu wa nchi.
Halikadhalika, walisisitiza haja ya kuendeleza mazungumzo ya mara kwa mara baina ya viongozi wa kisiasa ili kujenga uelewa wa pamoja na kushughulikia changamoto za kitaifa kwa njia ya mazungumzo na ushirikiano, kwa kutanguliza maslahi ya wananchi na maendeleo ya Taifa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais pamoja na Wagombea Wenza wa Vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya Mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea Wanawake katika nafasi ya Urais pamoja na Wagombea Wenza wa Vyama vya Siasa 16 vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha na Wagombea wa nafasi ya Urais Wanawake ambao ni Saum Hussein Rashid kutoka chama cha UDP na Mwajuma Noty Mirambo kutoka chama cha UMD walioshiriki Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba, 2025 mara baada ya mazungumzo yao, Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 31 Machi, 2026.Mazungumzo hayo yanaakisi dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuendeleza mawasiliano ya wazi na ya kujenga miongoni mwa viongozi wa kisiasa, kwa lengo la kuimarisha maridhiano na mshikamano wa kitaifa.
Tags
Dr Samia Suluhu Hassan
Habari
Ikulu Magogoni Dar es Salaam
Wagombea Urais 2025
Wagombea Wenza 2025
