DAR-Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba,Aden Rage amesema kuwa,ana imani kubwa kwa Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani uliotokea wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025 kwani tume hiyo imejengwa na watu wengi wenye uwezo mkubwa zaidi.
Amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari na kueleza kuwa, tume hiyo ina watu wenye heshima kubwa ulimwenguni na hata taasisi na jumuiya za Kimataifa.
Rage amewahimiza Watanzania kutosikiliza ama kufuata maneno ya kwenye mitandao kuhusu yaliyotokea Oktoba,29 na badala yake wasubiri ripoti ya Tume Huru ya Uchunguzi ili kupata ukweli wa kina.
.jpeg)