Rais wa zamani wa Liberia awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR-Rais wa zamani wa Liberia, Mheshimiwa Ellen Johnson Sirleaf ambaye pia ni Mlezi wa Mtandao wa Wanawake Viongozi barani Afrika African Women Leaders Network -AWLN) amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Aprili 19 hadi 22 Aprili 2026.Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),Mhe. Sirleaf alilakiwa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. James Millya.
Akiwa nchini Mheshimiwa Sirleaf anatarajia kushiriki mkutano wa Kamati ya Uongozi ya AWLN, kukutana na viongozi wa Serikali,viongozi wa dini, asasi za kiraia, vyama vya siasa na Wanawake kwa lengo la kukuza usawa wa kijinsia, utawala bora, kuhamasisha Wanawake na maendeleo jumuishi.

Mtandao wa Viongozi Wanawake Afrika (AWLN), ulianzishwa kwa lengo la kukuza sauti na ushawishi wa wanawake katika nafasi za uongozi, unaendelea kuwa chombo muhimu katika kuunda sera zinazowezesha wanawake kisiasa, kiuchumi na kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here