DAR-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetangaza mabadiliko ya ratiba za treni za kisasa (SGR) kati ya Dar es Salaam na Morogoro, yatakayoanza kutumika rasmi Aprili 18, 2026.
Kwa mujibu wa ratiba mpya, treni zitaondoka Morogoro saa 3:50 asubuhi kuelekea Dar es Salaam na kuwasili saa 5:40 asubuhi. Safari nyingine itaondoka Dar es Salaam saa 6:20 mchana na kuwasili Morogoro saa 8:05 mchana.
Aidha, treni itaondoka Morogoro saa 8:25 mchana kuelekea Dar es Salaam na kuwasili saa 10:10 jioni, huku safari ya mwisho ikiondoka Dar es Salaam saa 10:30 jioni na kuwasili Morogoro saa 12:29 jioni.
TRC imeeleza kuwa huduma hiyo itatolewa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumapili, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha usafiri wa reli na kuongeza ufanisi kwa abiria.
