Serikali yaeleza dhamira ya kuwawezesha vijana kiuchumi

ASIA SINGANO NA
JOSEPHINE MAJURA

SERIKALI imeeleza dhamira yake ya kuendelea kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), katika Mahafali ya 20 ya Shule ya Sekondari ya Thaqaafa wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (kulia), akijadiliana jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, (katikati), pamoja na Meneja wa Shule ya Sekondari Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, alipowasili katika Shule ya Sekondari Thaqaafa, kwa ajili ya Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya shule hiyo jijini Mwanza.

Alieleza kuwa, Serikali inaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupitia Sera na mipango mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ili kuhakikisha kuwa vijana wanapata fursa za kuendeleza vipaji vyao na kuchangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

"Dunia ya sasa inahitaji vijana wanaoweza kutatua changamoto kwa ubunifu, hasa katika nyanja za uchumi, teknolojia na ujasiriamali," alisema Mhe.Munde.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (kushoto), akiteta jambo na Meneja wa Shule ya Sekondari Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya shule hiyo iliyopo wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika mahafali hayo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), (kulia), akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi, wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza.

Amewaasa vijana kuendelea kuwa na nidhamu na uadilifu kwakuwa Taifa linahitaji vijana wenye misingi imara ya maadili, wanaoweza kusimamia rasilimali za nchi kwa uwajibikaji na weledi.
Wahitimu wa Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Thaqaafa, wakimsikiliza Mgeni Rasmi wa Mahafali ya 20 ya shule hiyo, Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (hayupo pichani), alipokuwa akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo jijini Mwanza.
Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Thaqaafa, Bw. Jafar Kubelabo, akizungumza katika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiwatunuku vyeti na zawadi wanafunzi waliyofanya vizuri kwenye masomo mbalimbali, wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa Mgeni Rasmi katika mahafali hayo.Kwa upande wake Meneja wa Shule ya Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi, amewasisitiza wazazi kuendelea kushirikiana na walimu na Uongozi wa shule kufuatilia maendeleo ya wanafunzi ili kujua mwenendo wa tabia ambazo zina athari katika masomo yao.
Picha za matukio mbalimbali wakati wa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita katika Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza.
“Shule imejipanga kutoa elimu bora ikiwa na matokeo mazuri kwa kila mwaka, tunavyofanya mawasiliano na mzazi ni kwamba atoe ushirikiano ili mtoto apate kitu kinachostahili,’’alisema Bw.Hayeshi.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (katikati,walioketi), Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mhe. Amina Makilagi (kushoto kwake, walioketi), Meneja wa Shule ya Sekondari Thaqaafa, Bw. Idrisa Hayeshi (kulia kwake), wakiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa shule ya Sekondari ya Thaqaafa, baada ya kumalizika Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, wilayani Nyamagana jijini Mwanza alipokuwa Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo.
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe, Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), akiagana na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mhe. Amina Makilagi, baada ya kumalizika kwa Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Thaqaafa, jijini Mwanza alipokuwa mgeni Rasmi katika Mahafali hayo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF- Dodoma).

Shule ya Sekondari Thaqaafa imeadhimisha Mahafali ya 20 ya Kidato cha Sita ambayo yalihudhuriwa na wahitimu (50).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here