DAR-Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Mheshimiwa Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema kuwa, kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi wa Matukio ya Vurugu zilizotokea baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ni taswira nzuri ambayo nchi imeonesha kuwa inao uwezo wa kushughulikia na kutatua changamoto zake yenyewe bila kuingiliwa na watu wa nje.
Prof.Ibrahim amesisitiza kuwa,tume hiyo ni huru na haiingiliwi na taasisi au mtu mwingine wa nje na ni tume ya Kimataifa,kwani inaongonzwa na sheria za Kimataifa na sio za Tanzania pekee na imesheheni watu wabobevu wenye uzoefu wa kazi za Kimataifa.
.jpeg)