Uchumi wa Tanzania wapewa mwelekeo mpya katika Mkutano wa IMF

WASHINGTON D.C-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo anayesimamia Idara ya Afrika, Bw. Abebe Selassie, katika Ofisi za makao makuu ya IMF, jijini Washington D.C Nchini Marekani, pembezoni mwa Mikutano ya Kipupwe ya Benki ya Dunia na IMF (2026 IMF/WBG Spring Meetings) inayofanyika, Jijini humo, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali yanayohusu uchumi wa Tanzania
Mhe. Balozi Omar, alieleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kusimamia uchumi wake unaoendelea kukua lakini pia inachukua hatua mbalimbali madhubuti za kuhakikisha kuwa uchumi unaendelea kuwa imara licha ya misukosuko hiyo
Mikutano hiyo ya uwili (bilateral meetings), imewashirikisha pia Waziri wa Nchi-Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Juma Malik Akil, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Dkt. Elsie Kanza, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Fedha na Mipango Zanzibar, Bw. Aboud Hassan Mwinyi, Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba, Msaidizi wa Katibu wa Baraza la Mawaziri, Bw. Francis Mossongo na maafisa wengine wa Serikali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here