Ushirikiano wa sekta chachu ya mafanikio ya Afya Moja

KAGERA-Timu ya wataalam kutoka sekta za afya, mifugo, mazingira, wanyamapori na kilimo imekutana katika Halmashauri ya Wilaya ya muleba mkoani Kagera kwa lengo la kuandaa Mpango wa Mkoa wa Afya Moja ambao utatumika kubaini rasilimali zitakazosaidia kutatua changamoto na vihatarishi vya afya ya binadamu, wanyama na mazingira.
Afya Moja inawaleta wadau pamoja kwa lengo la kuunganisha nguvu kutoka sekta mbalimbali ili kuhakikisha dhana hiyo inatekelezwa kwa matendo huku ikizaa matunda yanayotarajiwa kwa kuzingatia malengo ya kuanzishwa kwake.
Ofisi ya Waziri Mkuu yenye jukumu la kuratibu shughuli za Serikali, imebeba dhana hiyo kwa kuhakikisha inawashirikisha wadau wote muhimu huku ikiwa kinara katika kuivusha dhana ya Afya Moja nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here