Waziri Kombo aagana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Comoro

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana na kumuaga Balozi mteule wa Tanzania nchini Comoro, Mhe. Salim Othman Hamad, katika kikao kilichofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, Waziri Kombo amemtaka Balozi Hamad kutumia ipasavyo diplomasia ya uchumi ili kuimarisha mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Comoro, pamoja na kukuza sekta ya utalii.

Akisisitiza umuhimu wa kutumia nafasi hiyo kuibua fursa mpya za kiuchumi zitakazowanufaisha wananchi wa pande zote mbili.
Vilevile, Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza ushirikiano wa kidiplomasia uliopo kati ya Tanzania na Comoro, akihimiza uwakilishi madhubuti unaolenga kulinda na kukuza maslahi ya Taifa.

Kwa upande wake, Mhe. Hamad amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa imani na dhamana aliyompa ya kuiwakilisha nchi, na kuahidi kuitumikia Tanzania kwa weledi na uadilifu.
Kabla ya uteuzi wake, Mhe. Hamad alikuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia masuala ya siasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here