ISTANBUL-Wageni mbalimbali wanaohudhuria mkutano wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) wa 152 mjini Istanbul wamefurika katika Banda la Tanzania na kujionea vivutio mbalimbali vya Tanzania na wengi wakijiandikisha na kuthibitisha kushiriki mkutano wa 153 wa IPU utakaofanyika mkoani Arusha nchini Tanzania Oktoba,2026.
Zaidi ya Wabunge 2000 wa Mabunge ya Dunia wakiongozwa na maspika wa Mabunge yao wanategemewa kuhudhuria mkutano huo.
