DAR-Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), John Mrema amesema kuwa,kwa sasa ana matumaini makubwa na Tume ya Kuchunguza Matukio Wakati na Baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 chini ya Mhe.Jaji Mohamed Chande Othman kwa sababu tume hiyo ina watu weledi sana.
Mrema ameongeza kuwa,tume hiyo imeundwa na Rais kwa ajili ya kuwasaidia watanzania na imani yake ni kuwa itafanya kazi nzuri.
