Waziri wa Mambo ya Nje wa Belarus awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR-Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Belarus, Mheshimiwa Maxim Ryzhenkov, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu kuanzia Aprili 28 hadi 30, 2026, kufuatia mwaliko wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo.
Mheshimiwa Ryzhenkov amewasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, ambapo alipokewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe, pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Belarus nchini Mhe.Dzmitry Krasouski.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Ryzhenkov anatarajiwa kufanya mazungumzo ya pande mbili na mwenyeji wake, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo, Aprili 28, 2026, jijini Dar es Salaam. 

Aidha, atakutana na viongozi wengine wa Serikali kwa lengo la kuendeleza na kupanua ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.
Ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Belarus pamoja na kukuza ushirikiano wa kiuchumi katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here