NA DIRAMAKINI
MAHAKAMA ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imemuhukumu kwenda jela miaka 20 aliyekuwa Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ruvu Remit wilayani humo, Bw.Godbless Felix Mollel kwa makosa ya uhujumu uchumi.
Hukumu hiyo imetolewa Mei 28,2026 na Hakimu Mwandamizi Onesmo Nicodemos katika shauri la uhujumu uchumi namba 22415/2025.
Awali, mshtakiwa alishtakiwa kwa makosa ya ufujaji na ubadhirifu kinyume na kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa sura ya 329, kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022 kikisomwa pamoja na aya ya 21 jedwali la kwanza kifungu cha 57 (1) na 60(2) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi na makosa ya kupanga sura ya 200 R:E 2022.
Sambamba na kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258,265 na 270 vya Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2023.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kwa kosa la kwanza la ufujaji na ubadhirifu.
Aidha,katika kosa la pili la wizi akiwa mtumishi wa umma, mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani.
Hivyo,kwa makosa yote mawili mshtakiwa amepewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka 20 gerezani kwa pamoja.
Pia,mshtakiwa ameamriwa kurejesha kiasi cha shilingi 3,300,000 alichokifanya ubadhirifu katika akaunti ya Benki ya Maendeleo ya Kijiji cha Ruvu Remit.
Shauri hilo lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Wakili Faustin Mushi.
Tags
Habari
Jela Miaka 20
Kataa Rushwa
Mahakamani Leo
PCCB Tanzania
Ruvu Remit
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
.jpg)