BoT yatoa leseni kwa benki mpya ya huduma ndogo za fedha Dar es Salaam

NA DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa leseni ya kibenki kwa Radiance Microfinance Bank Limited,hivyo kuiruhusu kuanza kutoa huduma za kibenki kama benki ya huduma ndogo za fedha nchini.
Kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa leo Mei 22,2026 na Naibu Gavana anayeshughulikia Uthabiti na Usimamizi wa Sekta ya Fedha,Sauda K. Msemo,BoT imesema leseni hiyo ilianza kutumika rasmi Mei 4.2026.

Makao makuu ya benki hiyo yatakuwa katika Kiwanja Na.16/1, Elia Complex katika makutano ya Mtaa wa Zanaki na Barabara ya Bibi Titi jijini Dar es Salaam.

Benki Kuu ya Tanzania imeeleza kuwa,hatua hiyo ni sehemu ya wajibu wake wa kusimamia na kudhibiti taasisi za kifedha nchini.

Mwaka huu Benki Kuu ya Tanzania inaadhimisha miaka 60 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1966.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here