INEC yatoa maamuzi rufaa mbili za wagombea udiwani Kata ya Bwongera wilayani Chato

NA DIRAMAKINI

KWA kuzingatia masharti ya kifungu cha 65(7) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani, Sura ya 343, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema imepokea rufaa tano za wagombea Udiwani wanaopinga uamuzi wa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi wa Kata ya Bwongera iliyopo Halmashauri ya Chato mkoani Geita wa kutowateua kuwa wagombea.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Mei 15,2026 na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC),ndugu Kailima Ramadhani.

Ameeleza kuwa,katika kikao chake maalum kilichofanyika Mei 15,2026 Tume imesikiliza rufaa mbili kati ya rufaa tano zilizowasilishwa na kuzikubali.

Rufaa ya kwanza ni ya Anastazia Peter Bampiga mgombea Udiwani kupitia Chama cha UPDP dhidi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Bwongera.

Aidha, rufaa ya pili ni ya Ramlath Ramadhan Abdul mgombea Udiwani kupitia Chama cha N.I.D dhidi ya Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi Kata ya Bwongera.

"Hivyo, wagombea tajwa, wamerejeshwa katika orodha ya wagombea Udiwani katika kata husika na waendelee na taratibu za kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani utakaofanyika Juni 1,2026."

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,rufaa tatu zilizobaki zitasikilizwa na kutolewa uamuzi katika kikao cha Tume kitakachofanyika Mei 18, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here