Kamati ya Uratibu ya Mradi wa SOFF yakutana jijini Dodoma

DODOMA-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), kwa kushirikiana na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), walifanya kikao kazi cha tano cha Kamati ya Uratibu wa Mradi wa SOFF (Systematic Observations Financing Facilit) katika Hoteli ya Morena jijini Dodoma.
Kikao hicho kiliwakutanisha wataalamu muhimu ili kupitia maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa SOFF na kujadili vipaumbele vya kimkakati kwa mwaka 2026, vinavyolenga kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wa shughuli za mradi.



Majadiliano yalijikita katika utekelezaji wa Mpango Kazi wa Mwaka 2026, ufuatiliaji na tathmini ya mradi, pamoja na shughuli za mawasiliano na uhamasishaji zilizopangwa kwa mwaka 2026. Kamati pia ilipitia maamuzi na maelekezo kutoka kikao cha Tatu cha Kamati Tendaji ya Mradi wa SOFF kilihofanyika Aprili 2026.
Wakizungumza katika ufunguzi, Wenyeviti wenza wa kamati hiyo, Dkt. Paschal Waniha kutoka TMA na Dkt.Abbas Kitogo kutoka UNDP, walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana kikamilifu ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika kwa wakati katika shughuli zote zilizopangwa za mradi wa SOFF Tanzania.

Aidha,kikao kilihitimishwa kwa wajumbe kutoa dhamira ya pamoja ya kuimarisha uratibu, kuharakisha utekelezaji wa shughuli zilizopangwa, na kuongeza ufanisi wa jumla wa mradi wa SOFF nchini Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here