Katika hatua nyingine muhimu ya kukuza rasilimali watu na kuimarisha ubunifu wa kiteknolojia nchini, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imepeleka wanafunzi 30 wa fani ya Uhandisi Umeme kwenda nchini China kwa ajili ya programu ya kubadilishana ujuzi wa kitaaluma.
Wanafunzi hao wameondoka Mei 14, 2026 kuelekea Chuo cha Cho-Ching, ambapo watasoma kwa muhula mzima wakishirikiana na wenzao wa China. Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano (MoU) yaliyosainiwa kati ya DIT na chuo hicho cha China, yakilenga kubadilishana maarifa, teknolojia na uzoefu wa kimataifa.
Akizungumza kabla ya safari hiyo, Naibu Mkuu wa DIT, Profesa Ezekiel Amri, aliwataka wanafunzi hao kuwa mabalozi wazuri wa Tanzania kwa kuzingatia nidhamu, kujituma katika masomo yao na kutumia vyema fursa hiyo adhimu.
Alisisitiza kuwa China ni miongoni mwa mataifa yaliyoendelea kwa kasi katika ubunifu wa teknolojia na miundombinu, hivyo wanafunzi hao wanatarajiwa kurejea na maarifa yatakayosaidia kutatua changamoto mbalimbali nchini.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






















