Magazeti leo Mei 16,2026

Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu-Kilifair 2026 yanatarajiwa kufanyika kwa siku nne mfululizo jijini Arusha kuanzia Juni 4, 2026, huku zaidi ya nchi 14 kutoka mataifa mbalimbali zikitarajiwa kushiriki.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha, Mkurugenzi wa Kilifair Promotion Co. Ltd, Tom Kunkler amesema maonesho hayo ya mwaka huu yamejikita zaidi katika ubunifu na utoaji wa fursa kwa wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi.

Amesema Tanzania imeendelea kuwa miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa utalii wa mikutano na biashara kutokana na mazingira ya kipekee yanayounganisha shughuli za biashara na vivutio vya asili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here