Tanzania imeendelea kuimarisha udhibiti dhidi ya ugonjwa wa Ebola kwa kushirikiana na nchi jirani ikiwemo Uganda, Rwanda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Kenya kupitia ushirikiano wa kikanda ili kudhibiti kusambaa kwa maambukizi ya Ebola.

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amesema hayo Mei 30, 2026 akiwa katika ziara mkoani Kagera kwa lengo la kukagua udhibiti na utayari wa kukabiliana na ugonjwa huo mipakani pamoja na vituo vya afya vya kutolea huduma za dharula akiambatana na timu kutoka Wizara ya Afya, OWM- TAMISEMI na Mkoa wa Kagera.
“Zaidi ya wasafiri elfu 75,000 wamefanyiwa uchunguzi katika mipaka mbalimbali nchini tangu kuongezeka kwa tahadhari za Ebola, huku takribani watu 45,000 wakifanyiwa tathmini ya kina zaidi kutokana na kuhisiwa lakini hakuna aliyebainika na ugonjwa wa Ebola,” amesema Dkt. Magembe.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















