Magazeti leo Mei 4,2026

Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa, amewaagiza watumishi wa afya nchini kuwa bajeti ya mwaka wa fedha 2026/27 inatakiwa kuonyesha mwelekeo wa taifa utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.
Mchengerwa amesema hayo Mei 3, 2026 wakati wa uzinduzi wa Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Wizara ya Afya jijini Mwanza.

"Katika bajeti ya 2026/2027, vipaumbele vyetu lazima vionyeshe mwelekeo wa Taifa. Kwanza, lazima tujiandae kikamilifu kwa utekelezaji wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote. Hili si suala la kadi pekee; ni suala la uwezo wa mfumo. Lazima miundombinu iwe tayari," amesema Mchengerwa.

Amesema ni lazima mifumo ya TEHAMA iwe imara pia dawa zipatikane na rasilimali watu wawepo pamoja na vifaa vya kufanyia kazi. Ameagiza mkazo katika uzalishaji wa ndani wa bidhaa za afya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here