Rais Dkt.Mwinyi akaribisha wawekezaji kutoka Uturuki kuwekeza Zanzibar

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameyakaribisha makampuni na wawekezaji kutoka Uturuki kuwekeza nchini, hususan katika sekta za biashara,nishati na miundombinu.Rais Dkt. Mwinyi ametoa wito huo leo Mei 2,2026 alipokutana na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Balozi Volkan Isikci, aliyefika Ikulu, Zanzibar, akiongozana na Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Balozi Bekir Geze.
Amesema, hatua hiyo itasaidia kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya nchi hizo mbili na kufungua fursa mpya za ushirikiano katika biashara na uwekezaji.

Aidha, amesisitiza umuhimu wa wawekezaji kuwekeza katika sekta za kimkakati zikiwemo nishati, kilimo, utalii, afya na miundombinu, pamoja na kuongeza thamani ya mazao ya ndani.
Kwa upande wake, Balozi Isikci ameihakikishia Zanzibar kuendelea kushirikiana na kuunga mkono juhudi za maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya,kilimo na utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here