Rais Kagame kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania kesho Mei 3,2026 ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ushirikiano wa pande mbili.
Kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, Rais Kagame atapokelewa na mwenyeji wake, Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, na kufanya mazungumzo rasmi yatakayolenga kukuza ushirikiano wa kiuchumi na kidiplomasia.

Tanzania na Rwanda zimeendelea kuimarisha mahusiano kupitia biashara na uwekezaji, huku Tume ya Pamoja (JPC) ikitumika kusimamia ushirikiano katika sekta mbalimbali.

Ziara hiyo inatarajiwa kuongeza kasi ya ushirikiano wa kikanda katika sekta za kimkakati.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here