DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na uhamisho wa viongozi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt.Moses Kusiluka,Rais Dkt.Samia amemteua Dkt.Eveline Munisi kuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, akichukua nafasi ya Rahma Riyadh Kisuo, ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Pia, Eliakim Maswi amehamishwa kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, kwenda kuwa Katibu Muuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu.
Aidha,Dkt.John Jingu amehamishwa kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Makundi Maalumu kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria.
