Serikali kujenga kituo cha kisasa cha uchenjuaji dhahabu Mwakitolyo

DODOMA-Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) imepanga kujenga kituo cha mfano cha kuchenjua madini ya dhahabu kwa kutumia teknolojia ya kisasa katika eneo la Mwakitolyo katika mwaka wa fedha 2026/27, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuwawezesha wachimbaji wadogo kuongeza tija na thamani ya madini yao.
Kauli hiyo imetolewa Mei 07, 2026 Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Madini, Mhe. Dkt. Steven Kiruswa wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Mwanahamisi Athuman.
Dkt. Kiruswa amesema ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya mkakati wa Serikali kupitia STAMICO wa kuwaendeleza na kuwaimarisha wachimbaji wadogo nchini. Ameeleza kuwa vituo vingine vya mfano vimejengwa katika mikoa ya Geita na Mara Mbeya.

Aidha, amesema mkandarasi wa utekelezaji wa mradi wa kituo cha Mwakitolyo tayari amepatikana na kwamba hatua za mwisho za kimkakati zikikamilika, ujenzi utaanza rasmi.
“Usanifu wa kituo hicho tayari umekamilika na kitakuwa na uwezo wa kuchenjua tani 120 za mbale kwa siku,” amesema Dkt. Kiruswa.

Ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kuongeza ufanisi katika shughuli za uchimbaji mdogo, kukuza ajira pamoja na kuongeza mchango wa sekta ya madini katika uchumi wa Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here