Tanzania yaunga mkono ubunifu mpya wa kifedha kuimarisha sekta za afya na usafiri

NA BENNY MWAIPAJA,
Congo Brazzaville

TANZANIA imeelezea msimamo wake wa kuunga mkono mbinu za fedha za mseto (blended finance) zitakazosaidia kuimarisha sekta za usafiri wa anga na afya barani Afrika, akieleza kwamba hakuna chanzo kimoja kitakachoweza kuziba mapungufu ya miundombinu ya bara hilo.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akizungumza kama Gavana Mbadala wa Tanzania wa Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki hiyo kuhusu uwezeshaji wa sekta ya usafiri wa anga na afya kupitia mada “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, uliofanyika katika Hoteli ya The Hilton, jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo, ambapo alisisitiza msimamo wa Tanzania wa kuunga mkono mbinu za fedha za mseto (blended finance) zitakazosaidia kuimarisha sekta za usafiri wa anga na afya barani Afrika, akieleza kwamba hakuna chanzo kimoja kitakachoweza kuziba mapungufu ya miundombinu ya Bara hilo.

Akizungumza kama Gavana Mbadala wa Tanzania kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba alisema suluhisho linalopendekezwa ni la vitendo, nafuu na linaendana na vipaumbele vya kitaifa vya Tanzania.

“Tunasisitiza matumizi ya rasilimali za umma na binafsi pamoja na dhamana na msaada kutoka kwa washirika. Hatuwezi kutegemea chanzo kimoja pekee,” alisema Dkt. Mwamba, akiongeza kuwa ni muhimu kuzingatia udhibiti wa deni linalozidi kukua katika nchi za Afrika.

Katika Mkutano huo, Dkt. Mwamba alisisitiza kuwa usafiri wa anga ni kichocheo cha biashara, utalii, uwekezaji na ukuaji wa kikanda na kwamba Tanzania inakaribisha uwekezaji wa ubunifu kwa ajili ya uboreshaji wa viwanja vya ndege, uimarishaji wa usalama, utengenezaji wa mifumo ya usafirishaji na kuunganisha safari za kikanda kwa ufanisi. Lengo ni kuifanya Tanzania kuwa kituo cha usafiri kwa Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, akiteta jambo na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, na Kamishna wa Idara ya Fedha za Nje, Bw. Rished Bade, wakati wa mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, uliofanyika katika Hoteli ya The Hilton, jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo.

Vilevile, kuhusu huduma za afya, Dkt. Mwamba alibainisha kuwa mifumo thabiti ya afya ni nguzo ya uzalishaji, raslimali watu na ustahimilivu wa kiuchumi inayohitaji fedha za kuaminika na nafuu kwa ajili ya dawa muhimu, vifaa vya kisasa na miundombinu ya afya inayoweza kustahimili mabadiliko ya tabianchi na mazingira.

Dkt. Mwamba alieleza mahitaji ya Tanzania kwa AfDB: kuendeleza msaada kwa ajili ya maandalizi ya miradi ili kuibua miradi inayoweza kuvutia wawekezaji, hususan kutoka sekta binafsi, upatikanaji wa dhamana na kuwa na masharti nafuu zaidi ya mikopo kutoka Taasisi za Fedha, ikiwemo AfDB.

“Tanzania iko tayari kushirikiana na AfDB na wadau wote kwa uwekezaji wa matokeo dhahiri kwa wananchi wetu,” alisema Gavana huyo.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, akimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (hayupo pichani), wakati akizungumza kama Gavana Mbadala wa Tanzania wa AfDB, kwenye mkutano ulioandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) kuhusu “Platform solutions to Africa’s Transformation: De‑risking Aviation and Health systems through Innovative Financing”, uliofanyika Hoteli ya The Hilton, jijini Brazzaville nchini Jamhuri ya Kongo.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Brazzaville, Jamhuri ya Kongo).

Mkutano huo uliofunguliwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, uliwaleta pamoja Wadau wa maendeleo, Mawaziri wa Fedha, Magavana wa Benki Kuu, wawekezaji na viongozi wa Serikali kuzungumza kuhusu njia za kuondoa vikwazo vinavyoweka hatari kwa wawekezaji na kuleta mbinu za upatikanaji wa fedha zenye tija kwa miradi ya usafiri na afya barani Afrika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here