Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa AfDB nchini Congo Brazzaville

DAR-Waziri Mkuu Dkt.Mwigulu Nchemba ameondoka nchini Mei 25, 2026 kwenda Brazzaville, Jamhuri ya Kongo kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa 61 wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB).
Mkutano huo utafanyika Mei 26 hadi 27, 2026, katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Kintele jijini Brazzaville, Jamhuri ya Kongo.

Mkutano huu ni jukwaa muhimu la majadiliano ya kimkakati kuhusu masuala muhimu ya maendeleo ya dunia, yakihusisha nchi wanachama, taasisi za kikanda na kimataifa ambalo linahusisha kuhamasisha upatikanaji wa rasilimali za fedha ili kuwezesha utekelezaji wa ajenda ya maendeleo ya Afrika na kuimarisha uwezo wa bara kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi na kifedha duniani.
Mkutano huo utawakutanisha wajumbe wapatao 3,000 ikiwemo Mawaziri wa Fedha na Magavana wa Benki Kuu za Afrika, Watunga Sera, wafanyabiashara, Taasisi za Kifedha, Washirika wa Maendeleo, Wajasiriamali pamoja na Wawekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here