Waziri wa Fedha ateta na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo Afrika (BADEA)

BRAZZAVILLE-Waziri wa Fedha, Mheshimiwa Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiteta jambo na Rais wa Benki ya Kiarabu ya Maendeleo Afrika (BADEA), Bw. Abdullah Kh Almusaibeeh, kando ya Mkutano Mkuu wa 61 wa mwaka 2026 wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na Mkutano Mkuu wa 52 wa Mwaka wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki hiyo (ADF), unaofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kintélé, kilichoko nchini Congo Brazzaville.
BADEA ni miongoni mwa Taasisi za Fedha zenye mchango mkubwa wa maendeleo nchini Tanzania kupitia misaada na mikopo nafuu ikiwemo kuwa sehemu ya wadau waliochangia utekelezaji wa mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe , mkoani Kilimanjaro na Tanga, ulioghatimu shilingi bilioni 407.07, ambapo shilingi bilioni 244.10 zimetolewa na taasisi za fedha ikiwemo BADEA na kiasi cha shilingi bilioni 162 kilitolewa na Serikali ya Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here