Waziri wa Fedha Balozi Omar ashiriki kikao cha maandalizi ya Mkutano wa NEISA jijini Kigali

KIGALI-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameshiriki kikao cha maandalizi ya ushiriki wa Mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA), ulioongozwa na Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi leo Mei 18, 2026, unaofanyika jijini Kigali nchini Rwanda kuanzia Mei 18-21, 2026.
Kikao hicho kimefanyika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania jijini Kigali na kuhudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Maji na Madini wa Zanzibar, Mhe. Seif Pandu, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba, Kaimu Naibu Katibu Wizara ya Fedha, Bw. Rished Bade, pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja wataalam kutoka Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC).
Mkutano wa NEISA unawakutanisha Viongozi wa Serikali, wataalam wa sekta ya nishati, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika na duniani kwa lengo la kujadili ubunifu, uwekezaji na matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here