Zanzibar yaahidi kutekeleza ushauri wa Benki ya Dunia kwa matokeo chanya Mradi wa PAMOJA

NA SAADA MBAROUK

WIZARA ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto imeahidi kutekeleza ushauri uliyotolewa na Benki ya Dunia (World Bank) katika utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania- PAMOJA unaotekelezwa na Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wakala wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi Zanzibar (ZEEA).
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,Abeida Rashid Abdallah akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Masuala ya Uendelevu wa kijamii ya ujumuishaji, Varalakshmi Vemuru kutoka Beki ya Dunia (World Bank) baada ya kumaliza kikao kifupi kilichofanyika jana ofisini kwake Kinazini, Unguja, kikao kimehusu mikakati ya utekelezaji wa Mradi wa Kukuza Usawa wa Kijinsia Tanzania- PAMOJA, unaotekelezwa na Wizara hiyo, kwa kushirikiana na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA).

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ndugu Abeida Rashid Abdallah baada ya kumaliza kikao kifupi kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, ofisini kwake Kinazini Unguja baina ya Wizara hiyo na ujumbe kutoka Benki ya Dunia.

Amesema kikao hicho kimetoa fursa ya kushauriana na kuelekezana katika utakelezaji wa Mradi wa PAMOJA ambao unafadhiniwa na Benki ya Dunia, kwa kipindi cha miaka mitano (2024- 2029), hivyo Wizara imepokea ushauri uliyotolewa ikiwemo kuwashirikisha jamii ili kuwajengea uelezwa kuhusu Mradi wa PAMOJA na kuongeza kasi ya kitendaji.
Ameleza kwamba Benki ya Dunia imetoa fedha shilingi za Kitanzania bilioni 33 kwa ajili ya Mradi wa PAMOJA ambao unalengo la kuwainua wanawake kiuchumi na kupunguza vitendo vya ukatili na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto.

Hivyo lengo la ujio huo ni kuona Mradi umefikia hatua gani katika utekelezaji na kushauriana njia sahihi za kuendeleza mradi huo.

Katibu Mkuu Abeida amesema katika mazungumzo yao pia wamekubaliana kuishirikisha zaidi jamii katika ngazi za chini ili kuwajengea uelewa kuhusiana na Mradi wa PAMOJA utakavyowanufaisha wanawake kiuchumi kupitia fursa za mikopo na masuala ya kupinga vitendo vya Ukatili na Udhalilishaji (GBV).
"Mradi huo utawainua kiuchumi vijana na wanawake kwa sifa ambazo zitakidhi vigezo vya kuwezesha kupata mikopo. Pia Mradi huo utajenga nyumba salama mbili moja Unguja na moja Pemba ambapo nyumba hizo zitatumika katika kuwahifadhi wahanga wa ukatili wa vitendo vya ukatili udahlishaji wa kijinsia,” amesema Abeida.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Uwezeshaji wananchi kiuchumi(ZEEA) ndugu Juma Burhani Mohd Amefahamisha Mradi huo hautowasaidia wanawake pekee bali na wanaume watawezeshwa ili kuwa na jamii ambayo itakuwa na mtazamo mkubwa wa kiuchumi na kubadilisha maisha ya wananchi hivyo muda sio mrefu wananchi watanufaika kupitia Mradi wa PAMOJA.
Amesema anaamini kupitia Mradi wa PAMOJA utaleta mabadiliko makubwa kwa wananchi kwani Mradi umelenga kuwainua wanawake kiuchumi pamoja na kuondoa vitendo vya Udhalilishaji katika jamii.

Kwa upande wa Benki ya Dunia akizungumza Mkurugenzi wa Masuala ya Uendelevu wa Kijamiii na Ujumuishi ndugu Valarakshmi Vemuru amesema Mradi huo unalenga zaidi katika masuala ya fursa za kiuchumi na kuwanusuru wanawake katika masuala ya unyanyasaji wa kijinsia, pamoja na Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya watoto (ECD) ili wanawake wapate muda mzuri wa kufanya shughuli zao za kiuchumi.
Aidha, ameitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia, Wazee na Watoto kuongeza kasi katika utekelezaji kwani Benki ya Dunia inapenda kutoa matokeo chanya ambayo yamebadilisha maisha ya wananchi kupita Mradi huo, Pia amesisitiza matumizi ya fedha yatumika vizuri kama ilivyopangwa katika utekelezaji wa Mradi wa PAMOJA unaofadhili wa Benki ya Dunia.

Mradi kwa Kukuza Usawa wa Kijinsi Tanzania- PAMOJA ni Mradi wa miaka mitano unafadhiliwa na Banki ya Dunia (World Bank) na unatekelezwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Kushirikiana na Wakala wa Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (ZEEA), umelenga kuwainua wanawake kupitia fursa za mikopo na kupinga vitendo vya Udhalilishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here