BoT yaendesha semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu dhamana za Serikali

NA MWANDISHI WETU

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeendesha semina kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu dhamana za Serikali, ikieleza umuhimu wake katika kugharamia miradi ya maendeleo na mchango wake katika kuimarisha uchumi wa nchi.
Akizungumza katika semina hiyo Alhamisi Juni 25, 2026, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa BoT, Bw. Emmanuel Akaro, alisema dhamana za Serikali zimekuwa nyenzo muhimu ya kuipatia Serikali rasilimali fedha zinazowezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema BoT inaendelea kuboresha mfumo wa uwekezaji katika Dhamana za Serikali ili kupanua wigo wa washiriki na kuongeza fursa za uwekezaji.
“Kwa sasa tunaandaa maboresho ya kanuni yatakayoruhusu ushiriki wa wawekezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani. Hivi sasa, washiriki wanaoruhusiwa ni Watanzania, raia wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC),” alisema Bw. Akaro.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mheshimiwa Mashimba Ndaki, aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa mchango wake katika kusimamia uthabiti wa uchumi wa nchi na maendeleo ya sekta ya fedha.
Ujumbe wa Benki Kuu uliongozwa na Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Laurent Deogratius Luswetula. 

BoT inaendelea kushirikiana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kupitia vikao vya kujengeana uwezo vinavyolenga kuwawezesha wabunge kufahamu kwa kina masuala mbalimbali ya sekta ya fedha, hatua inayochangia kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa sera za uchumi nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here