DODOMA-Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya uchukuzi na Lojistiki ya Bravo Group, Bi. Angelina Ngalula, akiambatana na jopo la wataalamu wake wakiwemo wahandisi na wasanifu majengo Juni 20, 2026 amefanya ziara ya kutembelea miundombinu ya Reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) kati ya Stesheni ya Magufuli jijini Dar es Salaam na Stesheni ya Bahi Mkoani Dodoma.
Akizungumza katika Steshejni ya Bahi, wakati wa majumuisho ya ziara yake hiyo, Bi. Angelina Ngalula, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta binafsi Tanzania (TPSF), kufuatia alichojionea uwekezaji mkubwa wa Serikali katika miundombinu hiyo, ameweka bayana Bravo kukata shauri kuwekeza katika maghala mahala ya utunzaji wa mizigo mahala hapo.Aidha,ameliomba Shirika la Reli Tanzania (TRC) kutopata tabu ya kutafuta mwekezaji kutoka nje ya nchi kwakuwa wako tayari kufanya hivyo.
Wakati huo huo, Mkurugenzi mtendaji huyo wa Bravo Group, ametoa rai kwa wafanyabiashara kwenye sekta ya Lojistiki, Viwanda na Biashara kuwa mustakabali (future) upo kwenye reli na treni akimaanisha kwamba usafiri wa reli utakuwa na nafasi kubwa zaidi katika maendeleo ya baadae ya uchumi, usafirishaji na ustawi wa jamii.


