Kombe la Dunia 2026:Lionel Messi aandika historia,afunga hat-trick yake ya kwanza na kusawazisha rekodi ya Miroslav Klose

NA DIRAMAKINI

NAHODHA wa timu ya taifa ya Argentina, Lionel Messi ameendelea kuthibitisha ubora wake katika soka la dunia baada ya kufunga hat-trick yake ya kwanza katika michuano ya Kombe la Dunia la FIFA 2026 na kuiongoza Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Algeria katika mchezo wa Kundi J.
Messi alikuwa nyota wa mchezo huo katika dimba la Kansas City nchini Marekani,baada ya kufunga mabao yote matatu ya Argentina katika dakika za 17, 60 na 76, matokeo yaliyoiwezesha timu hiyo kuanza kwa kishindo kampeni yake ya kutafuta taji la dunia.

Hat-trick hiyo imeingia katika vitabu vya historia ya Kombe la Dunia,kwani ni mara ya kwanza kwa mshambuliaji huyo mkongwe kufunga mabao matatu katika mechi moja ya fainali za michuano hiyo.

Aidha, mabao hayo yameongeza idadi ya mabao yake katika Kombe la Dunia kufikia 16, akifikia rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na nyota wa zamani wa Ujerumani, Miroslav Klose, ambaye ndiye aliyekuwa kinara wa mabao wa muda wote katika historia ya mashindano hayo.

Argentina ilianza mchezo kwa kasi na kutawala umiliki wa mpira huku Messi akifungua ukurasa wa mabao dakika ya 17 kwa shuti lililomshinda kipa wa Algeria.

Bao hilo liliipa Argentina utulivu na kuifanya iingie mapumzikoni ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilishuhudia Algeria ikijaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Argentina uliwanyima nafasi ya kufanya hivyo.

Messi aliendelea kuonyesha uwezo wake mkubwa kwa kuongeza bao la pili dakika ya 60 kabla ya kukamilisha hat-trick yake dakika ya 76 na kuhitimisha ushindi wa mabao 3-0.

Ushindi huo unaifanya Argentina kuanza vyema hatua ya makundi ya Kundi J na kuongeza matumaini ya kufanya vizuri katika michuano hiyo.

Vilevile, umeendelea kuthibitisha mchango mkubwa wa Messi ambaye licha ya uzoefu wake mkubwa bado anaendelea kuwa tegemeo kuu la taifa hilo katika mashindano makubwa.

Kwa kufikia mabao 16 ya Kombe la Dunia, Messi sasa amejiweka katika nafasi ya kipekee ya kuandika historia mpya ikiwa ataongeza bao lingine katika michezo ijayo ya mashindano hayo.

Wadau wa soka duniani sasa watakuwa wakifuatilia kwa karibu safari yake ya kuvunja rasmi rekodi ya Klose na kuwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Kombe la Dunia.

Pia,Hat-trick hiyo imeifanya Argentina kutuma salamu kwa wapinzani wake wa Kundi J huku Messi akiendelea kuonyesha kwamba bado ni mmoja wa wachezaji wenye ushawishi mkubwa zaidi katika soka la kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here