Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kizimbani kwa tuhuma za rushwa

NA DIRAMAKINI

KESI ya Jinai Na.12889/2026 imefunguliwa Juni 10,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida dhidi ya Mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba,Bw.Innocent Christopher Ntayomba ambaye ni Mhasibu.
Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka ya ubadhirifu na ufujaji kinyume na Kifungu cha 28(1) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Sura ya 329 Marejeo ya 2023, kutotii wajibu kinyume na kifungu cha 123 cha Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 Marejeo ya 2023.

Inadaiwa kuwa, kati ya Aprili 16, 2021 na Januari 16, 2023 mshtakiwa huyo alikusanya ushuru minadani kwa kutumia mashine ya POS na kushindwa kuwasilisha benki shilingi 23,492,000.

Mashtaka yalisomwa na Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Bi.Yvonne Munisi mbele ya Hakimu Mkazi Mahakama ya Iramba, Mhe.Luzango Khamsini.

Aidha,mshtakiwa alikana mashtaka yote na yupo nje kwa dhamana, ambapo kesi imeahirishwa hadi Julai 2,2026 kwa ajili ya hoja za awali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here