Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yafanya mazungumzo na ujumbe kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania

DODOMA-Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepokea Ujumbe na kufanya mazungumzo kutoka Ubalozi wa Japan nchini Tanzania.
Ujumbe huo umetembelea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliyoko Mtumba jijini Dodoma leo Juni 9,2026.

Akizungumza kuhusu ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa Masuala ya Kisheria Ndani ya Serikali, Bw. Ipyana Mlilo amesema kuwa,lengo la ujumbe huo ni kuaga pamoja kumtambulisha Mratibu mpya ambaye atakuwa anashughulia ushirikiano kati ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Ubalozi huo.
Alitumia fursa hiyo kushukuru Ubalozi huo kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kuomba kuendeleza ushirikiano huo hasa katika mafunzo ya kisheria.

Ujumbe huo uliongozwa na Mratibu anayemaliza muda wake, Bi. Yoshino Shibata ambaye alitumia fursa hiyo kutoa shukrani za dhati kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na kwa ushirikiano mkubwa na wa kihistoria waliompa katika kipindi chote cha utumishi wake nchini.
Kwa upande wake, Fumiyo Jin ambaye ni Matibu mpya ameahidi kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi hizi mbili katika kubadilishana uzoefu hususan katika nyanja za Kisheria.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Sheria Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Bi.Sylvia Matiku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here